ADVERT

30 August, 2008

TYVA yasaka neema kwa vijana kwa kuichambua sera na kutafakari programu bora kwa ustawi wa vijana wa Taifa zima

Mwakilishi toka Shule ya Mbezi Beach akitoa nukuu katika sera ya vijana ambayo ndipo hoja yake ilisimamia
"Asasi makini kama hii ya TYVA inapaswa kufanya kazi bega kwa bega na vijana hususan wa mashuleni pia ili iweze kuwa makinisha mapema na hatimaye tuje kuwa na kizazi makini cha vijana" Mwakilishi wa Tambaza akitoa hoja
Mwanaharakati Eben akichangia hoja katika mjadala wa sera ulioandaliwa na asasi ya TYVA nchini
Kijana mwakilishi toka shule ya Tambaza akisoma kwa makini sera mpya ya vijana ya mwaka 2007 iliyozinduliwa mwaka 2008
Injini Alex Mayunga hakuwa nyuma katika kushiriki harakati hizi adhimu za TYVA, hapa akiwa mnukuu wa yaliyoendelea.
Kamaradi Chambi Chachage akitoa mada ya hali ya sera ya vijana nchini
Washiriki wakifatilia kwa makini mjadala na mada toka kwa Kamaradi Chambi Chachage

Washiriki wakiwa makini kufatilia mjadala. Ndugu Elizabeth Riziki [Mwenyekiti TYVA Taifa] akiongoza mjadala, pembeni ni Mchambuzi wa sera na Mafiti wa kujitegemea Kamaradi Chambi Chachage
Kijana si umri pekee...ari, nia na haja ya dhati inaweza ikashinda hoja ya umri...hapa tunaweza muona Ndugu Richard Mabala akitoa hoja katika mjadala huu makini wa kuchambua sera na kutoa mstakabali wa hali ya vijana nchini.

Ni kipindi kirefu sana TYVA imekuwa ikiendesha harakati zake za dhati pasipo fungamana na kundi lolote katika kutetea ustawi bora, ushirikishwaji na ushiriki wa vijana katika vyombo kadha wa kadha vya kimaamuzi.




Sera ni miongoni mwa maeneo nyeti sana kuelekea ustawi huu adhimu ambao toka kuanzishwa kwakwe TYVA imekuwa na adhima ya kuufikia.


Ifahamike sera si kitu "object or thing" bali ni maono ya kimchakato hivyo basi hayana kikomo yaani ni endelevu! yanapaswa kujadiliwa na kuangaliwa mara kwa mara ili mwishowe tuweze kuwa na programu bora si tu kwa serikali bali hata wadau wengine wengi kama asasi za kiraia, vyama vya siasa zenye kulenga ustawi bora wa kijana!


Shime moto uliowasha na unaowashwa mara kwa mara na asasi ya TYVA usizimike bali uchukuliwe kama kaa la moto na kwenda kuwashia kwingine kokote Tanzania na hatimaye nchi nzima kuna waka moto....moto wa kudai haki!moto wa kudai mabadiliko!moto wa kudai ustawi bora kwa kijana wa kitanzania!moto wa kudai Taifa imara!

No comments: