ADVERT

05 August, 2008

Hivi tunakuza elimu kweli?

Wiki iliyopita kulikuwa na hekaheka na maandamano ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari!

Polisi wakaingilia kati na kuya"control"! ikiwa pamoja na kumwagiwa maji yale ya kuwasha...

Lakini nimekaa nikajiuliza sana...inakuwaje serikali wametumia nguvu nyingi sana kupambana na watoto wadogo sana yaani rasilimali watu na fedha zote kwa muda ule zilielekezwa kule vipi?yaani inashindwa kuingia akilini!!

Lakini vilevile tulikuwa wapi hatukuuliza swali ambalo nalitafakari sana kwa sasa kwa nini polisi kwa ujumla wao [wanajeshi nk] hawakulipa nauli wakati wanalipwa mshahara?kama hakuna mabasi yao je si wangeongezewa fedha kwenye mshahara wao?

Vipaombele vyetu ni wapi sana kama nchi?tunawaongezea nauli wanafunzi kitu ambacho kinakuwa mzigo kwa wazazi na hata wanafunzi na kupelekea baadhi kushindwa hii haitapelekea wengine kushindwa kuhudhuria shule??!!......Kwanini wanafunzi hasa hawa wa shule ya msingi kama serikali imeonelea wasilipe ada kwanini pia waachwe kutozwa nauli?

Mbaya zaidi nauli yao imepanda lakini bado wanafunzi wanaendelea kunyanyaswa na kuhangaishwa katika kupata usafiri hasa katika miji!!

Hebu tuikirie naidi ya mazoea!

No comments: