Kwa wale wapenzi wa kusaka ukweli, naamini kwa sasa hawana amani! hii yote ni baada ya kukamatwa kwa vijana wawili washoka ndugu Maxence Melo na Mike Mushi kwa sababu ya masuala ya mtandao wa Jambo Forums www.jamboforums.com
Ni habari za huzuni sana kwani hata kile ambacho watanzania wengi walikuwa wakijivunia kupata jamvi la kujadili masuala mbali mbali bila woga hata kama yakiwa yanawagusa wakuu mbali mbali wa nchi lakini ni katika kujenga na si kubomoa.
Lakini hii vilevile ni tishio na hatari kwa sekta iliyochukuliwa kama salama ya habari hasa za mtandaoni, tulitegemea ukweli usambazwe vyema na kwa usalama maeneo haya lakini wapi huu ni mfumo mwingine wa kumwagia tindikali na kukata kata mapanga.
Hii imeleta hofu kwa wale wasiopenda kupatikanaji wa ukweli na kufunguliwa macho wananchi.
Hakika ukweli utashinda daima!
Aluta Continua.
1 comment:
t's such a important site. imaginary, quite intriguing!!!
-------
[url=http://oponymozgowe.pl]Opony[/url]
[url=http://pozycjonowanie.lagata.pl]Pozycjonowanie[/url]
[url=http://katalog.acy.pl/zdrowie,i,uroda/opony,s,7505/]opony[/url]
Post a Comment