ADVERT

03 September, 2010

TYVA Yawahamasisha vijana Kupiga Kura!

TANZANIA YOUTH VISION ASSOCIATION

Asasi ya Tanzania Youth Vision Association, leo tarehe 3/10/2010 imezindua rasmi mradi wa kuhamasisha vijana kupiga kura unaoitwa; “KIJANA KURA YAKO 2010”.

Uzinduzi huo umefanyika shule ya Makongo jijini Dar es Salaam. Baada ya hapo asasi hiyo itaendeleza harakati zake katika shule nyingine za jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani. Pia asasi itaenda kwa vijiwe/kempu vya vijana mitaani kuwahamasisha vijana.

Sambamba na kuwafata vijana walipo, asasi imezindua pia blogu (www.kijanakurayako2010.wordpress.com )pia kundi katika mtandao wa kijamii wa Facebook kwa jina la “Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010”.

Mradi huu ni wa kujitolea, unaendeshwa na vijana wenyewe pasi ufadhili wa wahisani ama shirika lolote. Lakini, inashirikiana na mashirika yaliyotoa machapisho ya Elimu ya Mpiga Kura kusambaza kwa vijana.

Tunawahamasisha vijana wote watembelee mitandao na kuchangia kwa habari, picha nk.
Kijana Jitokeze Kupiga Kura 2010!

Frederick Fussi,
Katibu Mtendaji-Tanzania Youth Vision Association.

No comments: