ADVERT

25 July, 2008

Kwa Mwoga huenda Kicheko..Shujaa Kilio!

Leo ni siku ya Kukumbuka mashujaa waliopoteza uhai wao katika harakati za Taifa letu TANZANIA!

Wapo wengi sana waliomwaga damu toka enzi za vita ya majimaji ...vita ya dunia......Vita dhidi ya Idd Amin.....Mwembechai.....hadi uchaguzi mkuu wa 2000 [Huko Zenj si mnakumbuka baada ya uchaguzi umwagaji damu ulitokea]!

Je sasa tunao mashujaa wenye uchungu na nchi yetu?hilo ndilo swali la msingi la kujiuliza kila tufanyapo kumbukizi hii adhimu.

Taifa lahitaji mashujaa wengi sana wamwage damu zao kwa manufaa ya vizazi vijavyo..nani atadiriki?udhalimu unakithiri kila kukicha.

Pumzikeni kwa amani.

No comments: