ADVERT

22 July, 2008

Ya Kubenea si ya Kumezewa!

Ndugu zanguni,
Poleni sana kwa kunikosa kwa kipindi kirefu kidogo...ni katika harakati za mapambano hukoo usukumani!nilibahatika kuwa katika kundi "team" ya kuwafunda asasi za kiraia na waandishi wa habari chini ya mradi wa UNA-LVI unaoendeshwa na UNA-TZ.

Wiki iliyopita yaani ijumaa tulihabarishwa kuvamiwa kwa ofisi ya Mwanahasili na watu wanaosemekana ni maafisa wa polisi waliofika kumsachi yeye "Kubenea" na ofisini katika kusaka kile kinachoitwa nyaraka zozote ambazo zinaweza kuhusiana na taarifa za kibenki ambazo wanahisi Mwanahalisi wanazihodhi.

Ikumbukwe Ndugu yetu Kubenea alishawahi kukutwa na maswahibu akiwa na Ndimara ya kumwagiwa Tindikali shukrani kwa Mungu kwa kumjalia afya njema baada ya matibabu huko India.

Tunahitaji waandishi makini, jasiri na imara kama Kubenea kwa afya ya jamii yetu na uwanda wa habari wka ujumla.

Kila mwenye uwezo wa kutoa msaada kwa mwanaharakati huyu wa habari....kama ni wanasheria jamani kuweni nae...kama waandishi pia tangazeni kiufasaha kwa umma.

No comments: