ADVERT

25 July, 2008

Sakata la Muungano....mjadala au laana?

Si mara ya kwanza hoja ya MUUNGANO kuzuka na kuchachamaliwa....ikumbukwe enzi za G55 kundi la wabunge waliochachamalia mwanzoni mwa miaka ya 90 hoja hii inagwa mwisho wake mmh.

Sasa imeibuka tena na licha ya juhudi za hapa na pale kujadili hali bado ni tete....Mhe ameutupia mzigo wanasheria na chama kijadili na kutoa maoni zaidi.

Lakini nini hasa baadhi ya nyeti hapa ni uchambuzi;
Ndugu zanguni nimekaa sana na kuendelea kulitafakari huku nikipitia machapisho kadha wa kadha hususan juu ya aina ya muungano na kuuangalia muungano wetu.Pia nimejaribu kurejea kwenye historia ya nyuma na kujifunza hasa nini kilitokea na hivyo kuweza kuangalia wapi tunaelekea kwani kama tutjuavyo historia ni mwalimu bora sana.

Kwa manufaa ya wote ni bora turejee hii historia na kuangalia hasa kulikoni na muungano wetu;

Ni kweli usiopingika nchi kubwa “Tanganyika” iliamua kuua utaifa wao na kuuchukua umoja kwa ujumla yaani walikubali ki mkataba baada ya muungano kusiwe na nchi iitwayo Tanganyika ingawa Zanzibar inaendelea kupeta.

1. Muungano ulifikiwa kwa njia ya dharua kwani mazungumzo kati ya Hayati Abeid A. Karume na Hayati Julius K. Nyerere yalianza mnamo tarehe 20.04.1964 baada ya siku nne yaani 25.04.1964 kulitiliwa saini ya kuanzishwa kwa jamhuri ya Tanzania na jamhuri ikawa yaani 26.04.1964.

2. Ibara ya 5 ya mkataba na kifungu cha 7 inasema “On the commencement of the interim constitution of the United Republic, the Constitution of Tanganyika shall cease to have effect for the Government of Tanganyika as a separate part of the United Republic”

Utata unakuja hapa;

3. Kifungu cha 8[1] kinasema “….On and after Union Day the existing law of Tanganyika and of Zanzibar shall continue to be the laws in the territories of Tanganyika and Zanzibar respectively…….” Hapa iweje tusizione Tanganyika?yaani iliyeyukaje ns Zenj ikabaki?

Kwa kuwa hapakuwa na muda wa kutosha wa kuandaa katiba ya muungano, kwa hiyo katiba ilitoa nafasi ya kuteuliwa kwa tume ya kupendekeza Katiba ya Muungano na kuitishwa kwa Bunge la Katiba ndani ya mwaka mmoja kupitisha Katiba ya Muungano na baada ya hapo katiba ya Tanganyika ikagoma na kuwa katiba ya Muungano.Na kwa sababu ya dharura hiyo katiba ya Tanganyika ilichukuliwa na kufanyiwa marekebisho ya hapa na pale hususan kusushisha Muungano na kwani chini ya uwezo aliopewa Raisi wa Jamhuri ya Muungano na kifungu cha 5[2] cha sheria ya Muungano kwa kukifanyia marekebisho Katiba ya Tanganyika kwa njia ya Amri “Decree”.

Lakini hoja hii si mara ya kwanza kuibuka hususan Bungeni ikumbukwe kundi la wabunge maarufu kama G55 liliwahi kuibua hoja hii kwa kuilitaka Bunge lilidhie uwepo wa serikali tatu yaani serikali ya Tanganyika, Zanzibar na ya Muungano.Lakini wapi lilipo ishia sasa ni kama historia!!Hapa tunaweza waona watu kama Jenerali Ulimwengu kwani alikuwa miongoni mwa wabunge hao.

4. Tume ya Nyalali ilishawahi kufanya kazi ya kulitazama hili na kwa upana sana na kutoa mapendekezo kufuatana na upeo wao pia maoni ya wananchi ambayo wengi walipendekeza sana uwepo wa serikali tatu yaani ya Tanganyika, Zanzibar na Muungano.Lakini duuh kama kawaida utekelezwaji wa maoni mengi sana ya tume zetu mmmh utata hapa!Nitarudi tena endapo itaonekana haja ya kufafanua zaidi katika hili.

Ikimbukwe mapendekezo ya Tume ya Nyalali yalikataliwa na Chama Cha Mapinduzi “CCM”!Sasa je siku chama kingine kitakapo shika hatamu itakuwaje?

Hebu turejee maoni ya Waziri Mkuu Mhe. Pinda ya kuwaachia wanasheria wa serikali ya Tanzania na Zanzibar kujadili kwa kina na kuangalia vifungu vya kikatiba katika Muungano na ile ya Zanzibar vinavyogongana na kupendekeza marekebisho.

Nitarudi tena kuja kuzizungumzia vyema kesi ambazo zishawahi kuanzishwa kuhusiana na suala la muungano yaani ile kesi yaSMZ vs Machano Khamis na wenzake ya 1999 na Kesi ya Seif Sharif Hamad vs SMZ , Criminal Appeal No. 171 ya 1992.

Hakika walishasema mjadala ni njia muafaka wa kutatua matatizo zaidi ya kulazimisha kuyamaliza yaani kwa Nguvu ya Hoja badala ya Hoja ya Nguvu!Kwani kwa kufanya hivyo kila kukicha mjadala utaendelea kuibuka kwani hata Yesu aliwahi kusema “…..ukinizuia kusema basi mawe yataanza kunena…”!

Kuna sababu nyingi sana za kuwa na muungano lakini lazima tuwe na muungano bora.Hatuna shaka na mapenzi na lengo jema la waasisi wa Muungano wetu yaani Hayati Nyerere na Karume lakini inatoa afya zaidi kufungua macho na kutafakari zaidi kwani kama tunavyoona awali kujadili muungano ilikuwa kama kuwatusi ama kuwa msaliti lakini sasa watu wanachachamaa.

Ni hayo tu kwa sasa,

No comments: